1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA.Uganda yapongezwa juu ya suala la wakimbizi

20 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF1Z

Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya wakimbizi Antonio Guterres ameyatolea mwito mataifa ya Magharibi kuiga mfano wa nchi ya Uganda ambayo inawahifadhi maelfu ya wakimbizi kutoka mataifa jirani yenye mizozo.

Akiadhimisha siku ya wakimbizi kwa mara ya kwanza nje ya nchi yake tangu achukue wadhifa huo,Guterres alitembelea kambi za wakimbizi za kaskazini Mashariki mwa Uganda karibu na mpaka wa Sudan na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Alisema Uganda inastahili kukuigwa kwa mfano huo na mataifa ya magharibi amabapo suala la wakimbizi limekuwa gumu kutokana na wahamiaji haramu pamoja na ugaidi.