1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: waasi wa LRA wakubali msamaha nchini Uganda

10 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG96

Waasi wanaopigana na serikali ya Uganda sasa wanasema kuwa wapo tayari kukubali msamaha uliotolewa na serikali hiyo.

Rais Yoweri Museveni aliahidi kutoa msamaha huo ikiwa kiongozi wa waasi hao wa Lord’s Resistance Army Joseph Koni ataacha harakati za upinzani.

Mazungumzo ya kuleta amani baina ya serikali ya Uganda na waasi hao yanatarajiwa kufanyika jumatano ijayo katika jimbo la Juba kusini mwa Sudan.

Kauli ya waasi hao juu ya kukubali msamaha huo inakingamana na iliyotolewa hapo awali ya kuukataa .

Lakini wizara ya mambo ya nje ya Uganda imefahamisha kuwa viongozi wa Lord’s Resistance Army wamewasilisha kwenye wizara hiyo habari juu ya kukubali msamaha wa serikali.