KAMPALA. Uganda kupokea ruzuku kutoka Japan
22 Agosti 2005Matangazo
Serikali ya japan itaipa Uganda ruzuku ya dola milioni 3.7 kushughulikia maswala ya afya nchini humo.
Balozi wa japan nchini Uganda Ryuzo Kikuchi na waziri wa fedha na biashara wa Uganda Dr Ezra Suruma walitia saini makubaliano mwishoni mwa wiki iliyopita.
Fedha hizo zinatarajiwa kuikwamua pakubwa sekta ya afya nchini Uganda.