1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA-Afisa wa cheo cha juu wa jeshi atiwa mbaroni kwa kupinga mpango wa Rais Museveni kubadilisha katiba ya nchi hiyo.

30 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF8f

Jeshi la Uganda limesema limemtia mbaroni afisa wa cheo cha juu wa jeshi hilo,ambaye alitoa matamshi hadharani ya kupinga mpango wa rais Yoweri Museveni,wa kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo ambayo yatampa nafasi ya kusimama tena katika awamu ya tatu ya urais,wakati wa utakapofanyika uchaguzi mkuu mwakani.

Msemaji wa jeshi la Uganda,Meja Shaban Bantariza amesema kuwa Brigedia Henry Tumukunde,ambaye anawakilisha jeshi la Uganda Bungeni,alikamatwa kwa madai ya kukiuka taratibu walizojiwekea.

Meja Bantariza amesema kuwa Brigadia Tumukunde,ambaye kwa mbali anahusiana na Rais Museveni,atafikishwa katika mahakama ya kijeshi katika siku chache zijazo.

Brigedia Henry Tumukunde ambaye ni mbunge machachari,alitoa matamshi hadharani kuupinga mpango wa Rais Museveni wa kutaka kubadilisha katiba ya nchi itakayokuwa na manufaa kwa upande wake yatakayomuwezesha kusimama tena kugombea urais kwa kipindi cha tatu.Brigedia huyo alisikika hivi karibuni akisema kuwa anakusudia kustaafu jeshini,ingawa bado jeshi la Uganda halijamkubalia kufanya hivyo.