1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump huenda akateuliwa mgombea 'asiye rasmi' wa Republican

26 Januari 2024

Kamati ya Kitaifa ya chama cha Republican nchini Marekani, inatarajiwa kutafakari kuhusu azimio la kumteuwa Donald Trump kuwa "mgombea wa urais'' asiye rasmi wa chama hicho

https://p.dw.com/p/4bguL
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Mike Segar/REUTERS

Haya yanatokea ingawa ni majimbo mawili pekee yaliopiga kura, huku Trump akiwa mbali na idadi ya wajumbe inayohitajika kujipatia nafasi hiyo.

Hii ni kulingana na rasimu iliyoonekana jana na shirika la habari la AP.

Kuidhinishwa kwa Trump kutampa udhibiti zaidi wa chama cha Republican

Ikiwa Trump ataidhinishwa, hatua hiyo itaimarisha zaidi udhibiti wake kwa chama hicho na uendeshaji wa shughuli zake wakati ambapo balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley bado yuko katika kinyang'anyiro cha uteuzi huo wa chama.

Soma pia:Trump akaribia uteuzi wa chama chake huko New Hampshire

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya kitaifa ya chama cha Republican Ronna McDaniel tayari ameashiria kuunga mkono hatua hiyo.