1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUrusi

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki yaisimamisha Urusu

Josephat Charo
13 Oktoba 2023

Kamati ya Olimpiki ya Urusi imejibu ikisema uamuzi huo hauna tija na umechochewa kisiasa.

https://p.dw.com/p/4XUb1
Frankreich |  Olympische Ringe vor dem Eiffelturm
Picha: Apaydin Alain/ABACA/picture alliance

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC imeisimamisha mara moja kamati ya Olimpiki ya Urusi kwa kukiuka uhuru wa mipaka wa uanachama wa Ukraine kwa kuyatambua maeneo yaliyotekwa kinyume na sheria.

Hatua hiyo inakuja baada ya kamati ya Olimpiki ya Urusi kuyatambua mashirika kutoka maeneo manne ya Ukraine yaliyotwaliwa na Urusi tangu uvamizi wa Ukraine mnamo 2022.

Msemaji wa IOC Mark Adams amesema siku ya ufunguzi wa mkutano wa bodi ya utendaji ya kamati hiyo mjini Mumbai, India, kwamba kamati ya Olimpiki ya Urusi haina tena haki ya kuendesha shughuli kama kamati ya kitaifa ya Olimpiki, kama inavyoainishwa katika mkataba wa Olimpiki na haiwezi kupokea fedha zozote kutoka kwa kamati ya IOC.

Kamati ya Olimpiki ya Urusi imejibu ikisema uamuzi huo hauna tija na umechochewa kisiasa.