1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Kagame na wenzake wakumbuka mauaji ya kimbari ya mwaka 1994

7 Aprili 2024

Rais wa Rwanda ameongoza kumbukumbu ya miaka 30 tangu yalipotokea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyosababisha mauaji ya zaidi ya watu milioni 1 katika taifa hilo la Afrika

https://p.dw.com/p/4eWDC
Mauaji ya halaiki ya Rwanda
Watu zaidi ya 800,000 waliuwawa katika mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994Picha: SIMON MAINA/AFP

Amesema mambo yaliyopelekea mauaji hayo kutokea hayatopewa nafasi tena ya kujitokeza katika siasa za Rwanda. Rais huyo wa Rwanda ameongeza kuwa siasa za Rwanda haziegemei misingi ya kikabila wala dini mambo yanayoaminika pia kuchochea mauaji hayo.  

Kagame na mkewe waliwaongoza viongozi 37 waliofika katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari katika mji wa Kigali ambapo zaidi ya wahanga 250,000 wanaaminika kuzikwa huko.

Wanyarwanda wakumbuka miaka 30 ya mauaji ya kimbari

Zaidi ya siku 100 ya mauaji hayo yaliyoanza Aprili 7 mwaka wa 94, watutsi na wahutu waliojaribu kuwalinda waliuwawa kinyama na wahutu wenye msimamo mkali walioongozwa na jeshi la Rwanda na wanamgambo waliojulikana kama Interahamwe.