1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kadhaa hawajulikani walipo baada ya ajali ya meli Ujerumani

24 Oktoba 2023

Meli mbili za mizigo zagongana karibu na kisiwa cha Heligoland kilicho katika Bahari ya Kaskazini mwa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4Xwmp
Watu kadhaa hawajulikani walipo baada ya meli kugongana Ujerumani
Watu kadhaa hawajulikani walipo baada ya meli kugongana UjerumaniPicha: Park Young-seo/Yonhap/AP/picture alliance

Watu kadhaa hawajulikani walipo baada ya meli mbili za mizigo kugongana karibu na kisiwa cha Heligoland kilicho katika Bahari ya Kaskazini mwa Ujerumani.

Haya yamesemwa na kamandi kuu ya mabaharia kuhusu masuala ya dharura. Katika taarifa kamandi hiyo imesema meli hizo za Polesie na Verity zimegongana karibu kilomita 22 kusini magharibi mwa Heligoland na kusababisha meli hiyo ya Verity kuzama.

Mtu mmoja ameokolewa kutoka majini na anapokea matibabu huku wengine wakiwa bado hawajulikani walipo. Mamlaka zinasema meli ya Polesie iliyokuwa imewabeba watu 22 bado iko majini.

Meli ya Verity ilikuwa inatoka Bremen ba kuelekea katika mji wa Uingereza wa Immingham nayo Polesie ilikuwa njiani kutoka Hamburg kuelekea La Coruna Uhispania.