1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kaburi lililozikwa watu wengi lagundulika Donetsk

8 Oktoba 2022

Gavana wa kijeshi katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine, Donetsk,Pavlo Kyrylenko amesema wamegundua makaburi mengine 200 na kaburi la pamoja.

https://p.dw.com/p/4HvBB
Massenfgrab in Lyman
Picha: PAVLO KYRYLENKO/REUTERS

Jana jioni, gavana huyo amesambaza picha katika ukurasa wake wa telegram akionesha maafisa wa huduma ya dharura wakiwa wamevaa mavazi ya kujikinga katika eneo lililowekewa kizuizi.

Katika ukurasa wake huo Kyrylenko ameandika "kazi ya ufukuaji wa eneo hilo tayari imeanza." Mwishoni mwa juma lililopita Urusi imeyatelekeza maeno yake ya kimkakati katika jiji la Lyaman.

Kwa mujibu wa polisi katika eneo hilo idadi ya waliuwawa bado haijafahamika ingawa inaaminika watu hao walikuwa polisi pamoja na watu wengine wa kawaida wakiwemo ndugu wa familia moja. Ugunduzi huu ni baada ya mauwaji ya mji mwingine wa kusini-mashariki mwa Ukraine wa Zaporizhzhya.

Watu 11 wauwawa na wengine 21 wajeruhiwa Zaporizhzhya

Ukraine Krieg | Krankenhaus in Saporischschja
Mwanajeshi aliyejeruhiiwa mjini ZaporizhzhyaPicha: Emre Caylak/AFP

Kwa mujibu wa serikali ya Ukraine takribani watu 11 walikufa baada ya makombora ya Urusi kulenga makazi yao. Idara ya Ulinzi wa Raia ya Ukraine imesema watu wengine 21 waliokolewa kutoka katika kifusi cha majengo, huku wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Mkoa wa Zaporizhzhya ni mojawapo ya mikoa minne ambayo juma lililopita imenyakuliwa rasmi, pamoja na Kherson, Donetsk na Luhansk. Wanajeshi wa Urusi kwa sasa wanadhibiti karibu 70% ya eneo hilo, lakini si

mji mkuu wa mkoa Zaporizhzhya yenyewe.

Katika kipindi hiki ambacho hakuna dalili ya kumalizika kwa vita na kukiongezeka kwa majadiliano kuhusu kitisho cha nyuklia, Rais wa UkraineVolodymyr Zelensky jana Ijumaa alionekana kujizua kutoa kauli zake zenye utata za kujihami dhidi ya Urusi katika mahojiano yake kwa njia ya televisheni.

IMF yatagaza kutoa msaada wa dharura  wa dola bilioni 1.3 kwa Ukraine.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ljana Ijumaa limetangaza kuwa litatoa msaada wa dharura wa dola bilioni 1.3 kwa Ukraine kupitia mpango wake mpya wa msaada wa mzozo wa chakula. Fedha hizo zitaisdaia Ukraine katika kufanikisha dharura ya mahitaji ya malipo yake huku pia zikiwa kama kichocheo katika kusaidia katika jukumu muhimu la kuweika ustahimilivu kwa kwa wadai na wafadhili wa Ukraine.

Soma zaidi:Baraza la Haki la UN kumteua mchunguzi huru dhidi ya Urusi

Shiria hilo la fedha IMF limesema "Ukubwa na makali ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vilivyoanza zaidi ya miezi saba iliyopita vimesababisha mateso makubwa ya binadamu na maumivu ya kiuchumi. Pato la Taifa halisi linatarajiwa kupunguzwa kwa asilimia 35 mwaka 2022 ikilinganishwa na 2021 na mahitaji ya kifedha yanabakia kuwa makubwa sana. "

 Vyanzo: DPA/AFP