1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Washukiwa saba wa al-Qaeda wauwawa

24 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDIS

Wanajeshi wa Marekani na wa Afghanistan wamewaua washukiwa saba wa kundi la al-Qaeda mashariki mwa Afghanistan.

Jeshi la Marekani limesema lilifanya operesheni ya kumsaka na kumkamata mwanaharakati wa al-Qaeda kwenye kijiji cha Asmar katika mkoa wa Kunar.

Lakini maofisa wa Afghanistan kwa upande wao wamesema watu wote saba waliouwawa ni raia.