1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Vikosi vya NATO kuimarishwa Afghanistan

5 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEUo

Maafisa wa uchaguzi nchini Afghanistan wanasema matokeo ya mwanzo ya uchaguzi uliofanywa mwezi uliopita yakitazamiwa kupatikana siku ya Alkhamisi,yataonyesha kuwa wana-harakati wa kike na viongozi wa vita ni miongoni mwa wajumbe wanaoongoza.Matokeo rasmi ya uchaguzi yanatazamiwa kutangazwa Oktoba 22.Siku ya jumanne,Katibu mkuu wa Shirika la Kujihami la NATO,Jaap de Hoop Scheffer alipokuwepo Kabul alisema Shirika la NATO linatazamia kupeleka Afghanistan,wanajeshi 6,000 wengine katika eneo la matatizo kusini mwa nchi.Vikosi hivyo vitakuwa sehemu ya ISAF-tume ya inayosimamia amani nchini Afghanistan na hivyo kutakuwepo jumla ya wanajeshi 15,000 nchini humo.Ufaransa,Ujerumani na Hispania hazitaki kuviunganisha vikosi hivyo na operesheni nyingine inayoongozwa na Marekani kupambana na wanamgambo wa Taliban.Serikali ya Taliban nchini Afghanistan ilipinduliwa mwaka 2001.Ripoti nyingine yasema kuwa nchi jirani ya Pakistan imemkamata msemaji mkuu wa Taliban,Abdul Latif Hakimi.