1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya ASEAN yahofia mizozo mipya

7 Septemba 2023

Rais wa Indonesia Joko Widodo amewatolea wito viongozi wa dunia kutatua mizozo inayoendelea wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN.

https://p.dw.com/p/4W3UF
Indonesien | ASEAN-India Gipfel
Picha: Indonesian Presidential Secretariat Press Bureau

Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala ya usalama na biashara wakati kukiwa na ushindani unaoendelea kuongezeka baina ya mataifa makubwa.

Soma pia: China yajitetea katika mkutano wa ASEAN

Mkutano huo umezungumzia pia mvutano wa muda mrefu kuhusu masuala ya biashara na teknolojia, pamoja na mzozo wa bahari ya China Kusini, hatua ya viongozi wa kijeshi wa Myanmar kukataa kushirikiana na mpango wa amani wa ASEAN pamoja na hofu kuwa Korea Kaskazini inapanga kuipa silaha Urusi.

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, Waziri Mkuu wa China Li Qiang na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov wamehudhuria katika mkutano huo uliofanyika katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta chini ya uongozi wa mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo pamoja na nchi washirika zikiwemo Japan, Korea Kusini, India, Australia.