1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juba, Sudan ya kusini. LRA watishia kususia mazungumzo ya amani.

24 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9V

Kundi la waasi nchini Uganda la Lord’s Resistance Army , limetishia jana Jumamosi kujitoa katika mazungumzo ya amani , likiishutumu serikali ya Uganda kwa kuwazingira katika kambi moja kinyume na makubaliano ya kusitisha mapigano.

Maafisa wa LRA wamesema kuwa majeshi ya Uganda yamezingira eneo hilo, moja kati ya vituo viwili kusini mwa Sudan ambako majeshi ya waasi wanatakiwa kujikusanya chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano , lenye lengo la kumaliza vita vya kikatili vilivyoikumba Uganda kwa muda wa miongo miwili.

Hakuna taarifa rasmi kutoka serikali ya Uganda.