1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JUBA: Masharti ya LRA yakataliwa na serikali

20 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG5x

Serikali ya Uganda imekataa mapendekezo yaliyotolewa na kundi la waasi la LRA katika majadiliano yanayofanywa Juba nchini Sudan. Miongoni mwa mapendekezo hayo,ni kuvunjwa jeshi la taifa na waasi wa LRA walipwe fidia wakidai kuwa wamefanyiwa ukatili.Naibu waziri wa nje wa Uganda,Okello Oryem amesema,serikali mjini Kampala inakubali mwito wa kusitisha mapigano,lakini hatua hiyo inaweza kuchukuliwa baada ya kumalizika majadiliano ya amani tu. Msemaji wa LRA,Obonyo Olweny amesema,msimamo wa serikali unazusha shaka kama kweli serikali hiyo inataka kupata amani.