1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joto la kiasa linaendelea kughubika Warepublican

4 Februari 2021

Warepublican watalazimika kwenda kwenye rekodi, kumtetea au kumkemea Mwakilishi Marjorie Taylor Greene, ambaye amekosolewa na vyama vyote kukumbatia nadharia za njama za mrengo wa kulia.

https://p.dw.com/p/3ot0X
Marjorie Taylor Greene
Picha: picture-alliance/AP/J. Bailey

Leo Alhamisi bunge linatarajiwa kupiga kura muhimu ya kisiasa, ambayo itaamua ikiwa Mrepublican huyo wa jimbo la Georgia ataondolewa majukumu yake ya kamati, na kuongeza wasiwasi juu ya mbinu gani bora ya kisiasa itakayoweza kutatua mvutano ulioibuka katika chama cha Republican tangu Donald Trump aliposhindwa katika uchaguzi mkuu.

Wademokrat mapema wiki hii, walitoa muda wa mwisho kwa Warepublican kumvua Greene majukumu yake ya kamati na iwapo watashindwa basi watamvua wao wenyewe. Shinikizo la pande mbili liliibuka baada kiongozi wa wachache katika bunge la Seneti Mitch McConnell kumuita Greene "Muongo " na "saratani" kwa chama. Soma Ziadi Mvutano kati ya rais Trump na wademocrat unaendelea

Lakini kiongozi wa wachache katika baraza la wawakilishi Kevin McCarthy, siku ya Jumatano aliondoa uwezekano kuchukua hatua zozote dhidi ya Greene. Badala yake, aliwashutumu Wademokrat kwa "unyakuaji madaraka wa kichama" kwa kumlenga Greene, ambaye wakati mmoja alisema kampuni ya kifedha ya Kiyahudi huenda ilishiriki katika njama ya kusababisga moto wa msitu jimboni California kwa kutumia miale ya angani.

US-Capitol | Wiederaufnahme der Sitzung
Picha: Win McNamee/Getty Images

Azma ya kumvua madaraka Greene

Mwenyekiti wa kamati ya kanuni za bunge Jim McGovern,  amesema wanaazimia kumvua Greene wadhifa wake. Uamuzi wa McCarthy kumuunga mkono Greene unakuja wakati chama hicho kina mgawanyiko wa kifikra baada ya kushindwa kwa Trump.

Siku ya Jumatano, Wabunge wa Republican walizuia juhudi za wahafidhina kumng'oa Mwanachama wa Republican mwakilishi Liz Cheney kutoka jukumu lake la uongozi. Cheney, mtoto wa Makamu wa rais wa zamani Dick Cheney, alikuwa amewakasirisha wafuasi wa Trump kwa kupiga kura ya kumshtaki juu ya ghasia zilizoshudiwa katika majengo ya Bunge. Soma Zaidi Wademocrat watoa wito rasmi ili Trump aondolewe madarakani

	Weltspiegel 04.02.2021 | USA Washington Marjorie Taylor Greene, Republikaner
Marjorie Taylor GreenePicha: Joshua Roberts/REUTERS

Greene ameonyesha kuunga mkono wito wa vurugu dhidi ya Wademokrat, na taarifa za uwongo juu ya ufyatuaji risasi shuleni na nadharia kuwa Wademoktrat wanaendekeza unyanyasaji dhidi ya watoto.

Matamshi ya Greene

Nadharia za njama ambazo amekumbatia ziliibuka wakati wa mkutano wa kamati ya wabunge wa Republican siku Jumatano, Baadhi ya waliohudhuria walisema Greene aliomba msamaha kwa wenzake, ingawa kulikuwepo na wanaopingana na matamshi hasa aliyotoa.

Kinyume na taarifa hiyo, wiki za hivi karibuni kupitia mtandao wake wa Twitter, Greene ameapa kuwa hatarudi nyuma au kuomba msamaha na aliwataja wakosoaji wake kuwa wasaliti, wanaotumia shinikizo la wademokrat kumwadhibu kuhusiana na juhudi zake za kutafuta pesa kwa ajili ya kampeni yake.

 

/Afpe