1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

John Kerry afanya mazungumzo na mwenzake wa China

17 Julai 2023

Mjumbe maalumu wa Marekani anayehusika na masuala ya mabadiliko ya tabianchi, John Kerry, leo amefanya mazungumzo na mwenzake wa China, Xie Zhenhua, mjini Beijing na kufufua diplomasia iliyokwama.

https://p.dw.com/p/4TzNy
China | John Kerry trifft Xie Zhenhua
Picha: Valerie Volcovici/REUTERS

Haya yameripotiwa leo na shirika la habari la China, CCTV, bila ya kutolewa maelezo zaidi kuhusu mkutano huo.

Hapo jana, mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan, aliliambia shirika la habari la CNN kwamba, Kerry angeishinikiza China isijifiche nyuma ya aina yoyote ya madai kwamba ni taifa linaloendelea ili kupunguza kasi ya juhudi za kupunguza utoaji wa hewa chafu.

Soma pia:Mvua kubwa yasababisha maafa nchini Japan

Sullivan ameongeza kuwa kila taifa ikijumuisha China, lina jukumu la kupunguza utoaji wa hewa chafu na kwamba dunia inapaswa kuishinikiza China kuchukuwa hatua kali zaidi kupunguza utoaji wa hewa hiyo.