1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Watumishi wa idara ya uhamiaji wataka kugoma kazi

28 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDHN

Nchini Afrika ya Kusini,maafisa wa uhamiaji kwa mamia wamepanga kugoma kazi.Mgomo huo unatazamiwa kuanza siku ya Ijumaa.Makamu wa meneja mkuu wa Jumuiya ya wafanyakazi wa idara za bandari, viwanja vya ndege na vituo vya mpakani,Manie de Clerq amesema,mgomo huo umeitishwa kwa sababu idara ya mambo ya ndani haikutimiza ahadi za kuongeza mishahara zilizotolewa mwaka mmoja uliopita.Wakati huo huo msemaji wa idara ya mambo ya ndani,Nkosana Sibuyi amewaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wanatafuta njia bunifu ya kukabiliana na mgomo huo.