1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joe Biden athibitishwa kuwa rais ajae wa Marekani

15 Desemba 2020

Jopo la wajumbe maalumu lenye nguvu ya kumchagua rais wa Marekani, maarufu kama Electoral College limemthibitisha Joe Biden kuwa rais ajae wa urais wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/3mjEu
USA | Präsidentschaftswahl | Mehrheit der Wahlleute stimmt für Joe Biden
Picha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Hatua hiyo inatajwa kuifunga milango kwa mpinzani wake Donald Trump, katika jitihada zake za kisheria za kuyageuza matokeo ya uchaguzi wa 2020. Hatu hiyo inafanyika huku mteule huyo akimkosoa mpinzani wake huyo kwa maneno makali tangu kumalizika kwa uchaguzi kwa kumwita mpinga matakwa ya umma na mkaidi katiba ya nchi.

Wakati Biden akipiga kampeni ya kuunganisha taifa, baada ya uchaguzi uliowagawa Wamerekani, wajumbe kutoka majimbo yote jana Jumatatu, kwa matokeo stahiki ya kura za wajumbe zinazohitajika  270. Hatua hiyo maana yake ni kumsafishia njia sasa kuekea kuingia katika ofisi za Ikulu ya Marekani Januari 20.

Hatma ya Urais wa Marekani, kwa Trump itasalia kuwa ndoto

Kimsingi Biden alifikia hatua ya uhakika wa ushindi baada ya nyongeza ya kura 55 za jimbo la California. Na pia baada ya Hawaii kumfanya  kuongeza idadi ya kufikia jumla ya kura 306. Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump alipata 232.

Utaratibu wa kura za wajumbe, ambao umedumu kwa takribani miaka 200, umepiga msumari wa mwisho kwa kusema matakwa ya umma yamezingatiwa pamoja na kutokea purukushani za hapa na pale. Na Trump kukataa kukubali kushindwa.

Biden amshambulia vikali mpinzani wake Trump

Donald Trump
Rais wa sasa wa Marekani, Donald TrumpPicha: Kevin Dietsch/UPI/ newscom/picture alliance

Akizungumza baada ya tangazo la kutambuliwa kwa ushindi wake, Joe Biden alisema hatua hiyo inadhihirisha kwamba demkorasia ya Marekani imeshinda. Alisema watu wamepiga kura, na tuma imani na chombo chao cha uchagzi na hivyo uadilifu wa mfumo wao wa uchaguzi unasalia kuwa thabiti. Lakini pia alimkosoa kwa Rais Trump kwa kumwita mkaidi mwenye kuipa kisogo katiba na kutoheshimu matakwa ya umma.

Lakini pamoja na hatua hiyo lakini bado, msimamo wa Trump kuhusu lawama za kufanyika wizi wa kura bado unasalia palepale ambapo baada ya tako la wajumbe, alitangaza Mwanasheria Mkuu Bill Barr, ambae alitofautiana nae kuhusu madai yake matokeo ya uchaguzi, ataachana na wadhfa huo wiki ijayo. Kama ilivyo kawaida yake Trump aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, aliandika "Bill ataondoka kabla ya Krismass, kwa lengo la kutumia kipindi hicho na familia yake, na kwamba uhusiano wetu ulikuwa mzuri."

Soma zaidi:Kamati ya "Electoral College" kumchagua rasmi Biden 

Uchaguzi wa Marekani wa Novemba 3, uliingia katika kizungumkuti tangu kumalizia kwake, baada ya Rais Donald Trump pasipo kuwa na ushahidi kuendelea kutangaza na kulalamika kwamba kulifanyika udanganyifu mkubwa.

Vyanzo: AP/AFP/DW