1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAmerika ya Kaskazini

Trump bado anakabiliwa na kisiki kugombea urais Marekani

29 Desemba 2023

Jimbo la Maine limempiga marufuku rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kushiriki uchaguzi wa kuwateua wagombea wa urais katika uchaguzi wa hapo mwakani.

https://p.dw.com/p/4ahBP
Siasa na sheria | Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Picha: Andrea Renault/ZUMA/picture alliance

 

Maine limekuwa jimbo la pili kuchukua uamuzi kama huo, kufuatia jukumu la Trump katika tukio la uvamizi wa makao makuu ya Bunge la Marekani mnamo Januari 6, 2021 uliofanywa na wafuasi wake mjini Washington.

Mwezi huu, Mahakama Kuu ya Jimbo la Colorado ilitoa uamuzi wakumzuia Trump kuwania tena urais, hatua ambazo bila shaka zitapingwa katika Mahakama ya Juu ya Marekani.

Soma pia:Mahakama ya juu Michigan yakataa jaribio la kumuondoa Trump

Maamuzi ya majimbo yote mawili yametumia kifungu cha 14 cha Katiba ya Marekani, ambacho kinamzuia mtu aliyehusika na uasi kuwania Urais.