1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je,Umoja wa Ulaya unaweza kuvimaliza vita vya Libya?

21 Februari 2020

Umoja wa Ulaya wenye wasiwasi wa ongezeko la wahamiaji kuingia barani mwake kupitia Libya, umekubaliana kuanzisha mkakati mpya wa kupiga doria katika bahari ya Mediterania kuzuia uingizwaji wa silaha nchini Libya.

https://p.dw.com/p/3Y7dj

Libya inashuhudia mapambamo makali ya kuwania madaraka ya mji mkuu wa Tripoli, kati ya serikali ya mashariki inayoongozwa na Kamanda Khalifa Haftar na ile inayotambuliwa kimataifa ya upande wa magharibi (GNA).

Pande hizo mbili zinaungwa mkono na washirika tofauti wa mataifa ya kigeni. Kwa hali hiyo, Umoja wa Ulaya wenye wasiwasi na suala la ongezeko la wahamiaji barani mwake kupitia Libya, umekubaliana kuanzisha tena mkakati wa kuzuia uingizwaji wa silaha Libya kupitia vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Je, Ulaya pamoja na Umoja wa Mataifa wamejiandaa vipi kumaliza vita vya Libya? Na je, suala la wahamiaji linawanufaisha vipi wanaowania madaraka nchini Libya?

Mwongozaji kipindi:  Saumu Mwasimba

Wageni: Safii Sufiani – Mchambuzi wa siasa za Afrika Kaskazini, Cairo, Misri

Abdul-Rahman Mohammed -  Mhadhiri wa Chuo Kikuu, London

Barack Muluka – Mchambuzi wa masuala la Kimataifa na Uhamiaji, Nairobi, Kenya