1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Jeshi Pakistan lauwa wanamgambo 8 karibu na Afghanistan

27 Novemba 2023

Jeshi la Pakistan limesema vikosi vyake vimevamia maeneo wanamojificha wanamgambo katika ngome ya zamani ya kundi la Taliban kaskazini-Magharibi mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4ZVIW
Usalama | Askari jeshi wa Pakistan wakiwa katika doria
Askari jeshi wa jeshi la Pakistan wakiwa katika doriaPicha: Aamir Qureshi/AFP

Uvamizi huo ulichochea kuzuka mapambano makali ya kufyatuliana risasi ambapo wanamgambo wanane wameuwawa.

Katika taarifa yake iliyotolewa usiku wa kuamkia leo, jeshi hilo la Pakistan limesema operesheni yake iliyotokana na taarifa za kiintelijensia ilifanyika jana katika mkoa wa Kusini mwa Waziristan na kwamba wanajeshi walifanikiwa kukamata silaha na risasi.

Soma pia:Taliban yataka Waafghani walio Pakistan wasaidiwe

Hata hivyo hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu wanamgambo waliouwawa, ingawa mara zote  kundi la Taliban nchini Pakistan linalofahamika kama Tehreek e-Taliban hulaumiwa kwa mashambulizi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW