1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi lawakamata mawaziri wanne Sudan

25 Oktoba 2021

Wanajeshi wamevamia nyumbani kwa mshauri wa habari wa Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok na kumkamata mapema leo.

https://p.dw.com/p/428Q1
Aufstand im Sudan
Picha: REUTERS

Televisheni ya Al hadath imesema wanajeshi wa Sudan wasiotambulika waliwakamata mawaziri wanne wa serikali na raia mmoja mwanachama wa baraza kuu la serikali.

Duru zinasema kuwa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok amewekwa chini ya kifungo cha nyumbani.

Siku ya Jumapili, waandamanaji wanaounga mkono jeshi nchini Sudan walifunga kwa muda barabara kuu na madaraja katika mji mkuu Khartoum.

Mvutano umezidi kuongezeka kati ya majenerali na vuguvugu la kuunga mkono demokrasia lililochochea uasi dhidi ya rais wa zamani Omar al-Bashir.

Baadaye mchana, vikosi vya usalama viliwatawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na kufungua barabara zilizofungwa.

Video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha waandamanaji wakikimbia juu ya daraja na kwenye Mtaa wa Nile.

Haya yalijiri siku moja tu baada ya Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Pembe wa Afrika Jeffrey Feltman kukutana na viongozi wa kijeshi na kiraia mjini Khartoum kutafuta mwafaka katika mzozo huo.

Taarifa zaidi kufuata