1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yatangaza kukiteka tena kijiji cha Kusini-Mashariki

12 Juni 2023

Jeshi la Ukraine limetangaza kukiteka tena kijiji cha Kusini-Mashariki huku majeshi ya Urusi yakidai kufanya mashambulizi mengi katika eneo hilo

https://p.dw.com/p/4SSTB
Ukraine Krieg | Kämpfe um Bachmut
Picha: Sergey Shestak/AFP

Mshauri wa Rais Volodymyr Zelenskyy amedai watu sita wamejeruhiwa baada ya askari wa Urusi kuishambulia boti iliyokuwa ya waokozi na kuwajeruhi waru sita. Idadi hiyo ya watu ilikuwa ikitoka katika maeneo ya Ukraine ambayo yanadhibitwa na Urusi katika kipindi hiki ambacho pia kuna shida ya mafuriko katika maeneo hayo.

Urusi na Ukraine kubadilishana wafungwa

Katika hatua nyingine ya siku ya Jumapili Ukraine na Urusi kwa nyakati tofauti zilitoa taarifa ya kubadilishana idadi ya wafungwa wa vita. Urusi ilisema wanajeshi wake 94 waliachiliwa na kwa upande mwingine Waukraine 95 wameachiwa huru.