1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ujerumani na ugumu wa kupata askari wapya

2 Agosti 2023

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani jeshi linakabiliwa na matatizo makubwa ya kuvutia makuruta wapya katika wakati ambapo Berlin inataka kulifanyia mageuzi jeshi lake kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4UhEK
BdTD Abschlussübung Projekt "Ungediente für die Reserve"
Picha: Christoph Schmidt/dpa/picture alliance

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius, amesema leo kuwa jeshi la nchi hiyo linakabiliwa na matatizo makubwa ya kuvutia makuruta wapya katika wakati ambapo Berlin inataka kulifanyia mageuzi jeshi lake kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.Waziri Pistorius amekiri kuwa jeshi la Ujerumani, Bundeswehr linakabiliwa na changamoto hasa ya kuvutia makuruta vijana.Katika ziara aliyoifanya kwenye kituo cha kutoa mafunzo juu ya taaluma hiyo mjini Stuttgart, waziri huyo wa ulinzi amesema kuwa Ujerumani imeshuhudia upungufu wa asilimia saba mwaka huu ya usajili wa makuruta katika jeshi ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.Kwa muda mrefu, jeshi la Ujerumani Bundeswehr limekumbwa na ukosefu wa raslimali na ufadhili japo baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Kansela Olaf Scholz amelazimika kuongeza ufadhili kwenye jeshi hilo.