1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuendelea na UNMISS na Sea Guardian Sudan Kusini

25 Januari 2024

Jeshi la Ujerumani linatarajiwa kushiriki katika operesheni ya usalama wa bahari ya jumuiya ya kujihami ya NATO Sea Guardian, pamoja na ujumbe wa kulinda amani wa UN nchini Sudan Kusini, UNMISS kwa mwaka mwingine

https://p.dw.com/p/4be5l
Msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Hebestreit ambaye pia ni mkuu wa ofisi ya habari ya serikali
Msemaji wa serikali ya Ujerumani - Steffen HebestreitPicha: Jens Krick/Flashpic/picture alliance

Msemaji wa serikali ya ujerumani Steffen Hebestreit, amesema Jumatano mjini Berlin kwamba baraza la mawaziri nchini humo, limeidhinisha kuongezwa kwa muda wa kuhudumu wa misheni zote mbili hadi Machi 2025.

Shughuli zinazofanywa na misheni ya Sea Guardian na UNMISS

Sea Guardian hutumia meli na ndege kufuatilia shughuli katika bahari ya Mediterenia na inatarajiwa kukabiliana na ugaidi na kuingizwa kwa silaha haramu.

Soma pia: 2023: Mwaka wa changamoto kwa walinda amani wa UN Afrika

UNMISS iliibuka kutoka kwa misheni iliyotangulia UNMIS kwa kutangazwa uhuru na Sudan Kusini mnamo mwaka 2011 na inakusudiwa kusaidia katika mchakato wa amani na kulinda raia.

Bunge la Ujerumani Bundestag bado linapaswa kuamua kuhusu muda wa kuongezwa kwa operesheni hizo.