1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUingereza

Uingereza yawaweka wanajeshi wake katika tahadhari

25 Septemba 2023

Karibu wanajeshi 100 wa jeshi la polisi jijini London wamekataa majukumu ya kutumia silaha baada ya mwenzao kushitakiwa kwa mauaji ya kumpiga risasi kijana wa Kiafrika ambaye hakuwa na silaha.

https://p.dw.com/p/4WkyK
Polisi wa London akiwa katika moja ya harakati za kusimamia usalama huko Westminster, September 24,2023.
Polisi wa London akiwa katika moja ya harakati za kusimamia usalama huko Westminster, September 24,2023.Picha: Vuk Valcic/Zuma/picture alliance

Uingereza imeyaweka majeshi yake katika tahadhari baada ya iddai kubwa ya polisi wa London kukabidhi silaha zao wakimuunga mkono afisa mwenzao aliyeshitumiwa kwa mauaji ya kijana mmoja wa kiafrika.

Wizara ya ulinzi wa Uingereza imethibitisha kwamba kwa sasa itasaidia baadhi ya majukumu ya polisi na hususan ya kupambana na ugaidi.

Polisi wengi nchini humo kwa kawaida huwa hawabebi silaha na wachache ambao huruhusiwa kujihami na silaha huwa wamepatiwa mafunzo ya hali ya juu.

Kulingana na vyombo vya habari, karibu polisi 100 wa London wamejitenga na majukumu yanayohitaji silaha.

Polisi huyo aliyetajwa kama NX121 alishitakiwa kwa kumpiga risasi kijana wa kiafrika wa miaka 24, Chris Kaba, Septemba 2022, kesi inayorejesha madai ya ubaguzi wa rangi ndani ya jeshi hilo.