1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF waendelea kushambuliana

28 Novemba 2023

Wanajeshi wa Sudan na wanamgambo wa RSF wanashambuliana kwenye kingo za Mto Nile unaokatisha mji mkuu wa Sudan, Khartoum, katika wakati mapambano baina ya pande hizo hasimu yanazidi makali miezi minane tangu yalipozuka.

https://p.dw.com/p/4ZVYF
Vikosi vya Jeshi la Sudan
Mapigano kati ya Jeshi la Taifa na wanamgambo wa RSF yamesababisha maafa makubwa nchini Sudan tangu yalipozuka Aprili, 15, 2023.Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Mashuhuda wamesema makombora na mizinga vimefyetuliwa kati ya jeshi lenye kambi upande wa magharibi mwa mto Nile na wapiganaji wa RSF waliopo ukingo wa mashariki mwa mto huo.

Inaarifiwa mapambano hayo yamedumu kwa siku kadhaa sasa na baadhi ya maroketi yameanguka kwenye makaazi ya watu na kusabisha vifo.

Mapambano baina ya pande hizo mbili yamechachamaa pia kwenye jimbo la Darfur na wiki iliyopita wanamgambo wa RSF walidai kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya jimbo hilo.

Juhudi za upatanishi bado zimegonga mwamba katika kuutafutia ufumbuzi mzozo huo ambao tayari umewauwa karibu watu 10,000 na kuwalazimisha mamilioni wengine kuihama nchi hiyo.