1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Sudan lawafyatulia mabomu ya machozi waandamanaji

30 Novemba 2021

Vyombo vya usalama vya Sudan vimewafyatulia mabomu ya kutoa machozi, watu walioandamana kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita

https://p.dw.com/p/43fUM
Sudan
Picha: Marwan Ali/AP/picture alliance

Waandamanaji hao wanapinga mapinduzi pamoja na makubaliano yaliyomrejesha madarakani waziri mkuu aliyekuwa ameondolewa katika mapinduzi hayo.

Mashahidi wamesema maelfu ya waandamanaji walikusanyika katikati ya mji mkuu Khartoum, na baadaye walitembea kuelekea kasri la rais ambapo walikabiliana na maafisa wa usalama.

Maafisa hao walikuwa wamewekwa katika maeneo yanayolizunguka kasri hilo kuwazuia waandamanaji kulikaribia.

Wakati wa maandamanano yao, wanaharakati wa demokrasia walipaza sauti wakisema, "Hakuna ushirikiano, hakuna majadiliano, hakuna uhalali" huku wakiwataka wanajeshi kurudi katika kambi zao.

Mnamo Oktoba 25, mwanajeshi mwenye ushawishi zaidi nchini Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alimuondoa madarakani Waziri Mkuu Abdalla Hamdok, lakini alimrejesha wiki iliyopita kufuatia shinikizo kubwa kutoka ndani na nje ya nchi.