1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Sudan lakabiliwa na upinzani mkubwa

Saleh Mwanamilongo
28 Oktoba 2021

Maafisa wa serikali mjini Khartoum wameapa kutotii amri inayotolewa na kiongozi wa kijeshi huku wanaharakati wakihamasisha maandamano makubwa baadaye wiki hii.

https://p.dw.com/p/42Izy
Nach Militärputsch im Sudan
Picha: AFP

Maandamano yamefanyika tena mjini Karthoum,mji Mkuu wa Sudan ili kupinga uongozi wa kijeshi Maelfu ya watu wameingia mitaani kulaani kurejea kwa utawala wa jeshi na kutaka uongozi wa kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia urejeshwe.

Katika taarifa ilitolewa kwenye mtandao wa Facebook usiku wa kuamkia leo, maafisa wa wizara na idara za jimbo lenye watu wengi zaidi la Khatroum, ambalo linajumuisha mji mkuu na mji pacha wa Omdurman, walisema hawatojiuzulu au kusitisha majukumu yao.

Walitangaza mgomo wa jumla, kujiunga na vyama vya wafanyakazi katika sekta kama vile afya na usafiri wa anga, ingawa walisema watafanya kuendelea kusambaza unga, gesi ya kupikia na huduma ya matibabu ya dharura.

Soko kuu, benki na vituo vya kujaza mafuta huko Khartoum bado zilifungwa Alhamisi. Hospitali zilikuwa zikitoa tu huduma za dharura. Maduka madogo yalikuwa yamefunguliwa, lakini kulikuwa na muda mrefu wa foleni ili kununua mkate.

Soma pia:Burhan awaondoa mabalozi 6 kwa kukosoa mapinduzi Sudan

''Sitatambua uamzi wa kiongo wa mapinduzi''

Mwakilishi wa UN nchini Sudan ajitolea kupatanisha ufumbuzi wa kisiasa
Mwakilishi wa UN nchini Sudan ajitolea kupatanisha ufumbuzi wa kisiasaPicha: Marwan Ali/dpa/picture alliance

Balozi wa Sudan mjini Geneva, Ali Ibn Abi Talib Abdelrahman Mahmoud,aliapa siku ya Alhamisi kutoyatambua mapinduzi yaliyoongozwa na Jenerali Abdel-Fattah Buran, akiongeza kuwa nchi hiyo inakabiliwa na aina mbaya zaidi za ukandamizaji.

"Ninatangaza, kwa uwazi kabisa, kwamba sitatambua uamuzi wa kiongozi wa mapinduzi, ambayo kwa usiku mmoja, imeiondoa serikali halali kikatiba.",alisema Mahmoud.

Katika ishara ya kuendelea kuwaunga mkono viongozi waliotimuliwa madarakani, waziri wa mamao ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema kwenye ujumbe wake wa twitter kwamba alizungumza kwa simu na waziri wa mambo ya nje wa Sudan Mariam Sadiq al-Mahdi.

Blinken alisema aliliaani kukamatwa kwa viongozi wa kiraia Sudan na kujadiliana na Mahdi jinsi gani Marekani inaweza kusaidia vyema zaidi wito wa Wasudan wa kurejea kwa uongozi wa mpito wa kiraia.Kam

Soma pia:Kamata kamata yaendelea Sudan baada ya mapinduzi

Tishio kwa demokrasia ya Sudan

Mapinduzi yaliyofanyika siku nne zilizopita yametokea wiki kadhaa kabla ya kiongozi wa kijeshi, Abdul Fattah al-Burhan kukabidhi madaraka ya Baraza la uongozi kwa uongozi wa kiraia. Baraza hilo ndilo linalotoa uamuzi muhimu wa kuiongoza nchi na hatua ya kukabidhi madaraka ingelipunguza nguvu ya jeshi nchini humo. Baraza hilo lilikuwa na maafisa wa kijeshi pamoja na kiraia na serikali ya Hamdok ndio iliyokuwa ikiendesha shughuli za kiserikali.