1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Jeshi la Sudan lajitoa kwenye mazungumzo na upinzani

31 Mei 2023

Jeshi la Sudan limesitisha ushiriki wake katika mazungumzo ya kusitisha mapigano na adui wake - kikosi maalum cha wanamgambo wa RSF.

https://p.dw.com/p/4S0MW
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akitoa hotuba katika hafla ya kusaini mpango wa makubaliano ya amani kati ya utawala wa kijeshi na kiraia mjini Khartoum, Disemba 5, 2022.
Pande zinazohasimia nchini Sudan zimekuwa zimekuwa zikikiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kila wakati na kusababisha hali mbaya nchini humo.Picha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Duru za kidiplomasia za Sudan zimeeleza leo kuwa jeshi limechukua uamuazi huo kwa sababu waasi hawajawahi kutekeleza hata moja ya vipengele vya usitishaji vita wa muda mfupi ambao ulihitaji kujiondoa katika hospitali na majengo ya makaazi. Jeshi la Sudan limesema mara kwa mara RSF imekiuka makubaliano hayo yanayosimamiwa na Marekani na Saudi Arabia. Siku ya Jumatatu Marekani na Saudi Arabia zilisema mahasimu hao wamekubaliana kuongeza siku tano zaidi za kusitisha mapigano ili kuruhusu shughuli za kiutu. Akivitembelea vikosi vyake katika mji mkuu, Khartoum, mkuu wa majeshi ya Sudan, Abdel Fattah al-Burhan amesema jeshi liko tayari kupigana hadi lipate ushindi.