1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Sudan laendelea kufunga anga

31 Julai 2023

Mamlaka ya safari za angani nchini Sudan imerefusha amri ya kulifunga anga la nchi hiyo hadi Agosti 15, isipokuwa tu kwa ndege za msaada wa kiutu na za kuwahamisha watu wanaokimbia mapigano kati ya pande hasimu.

https://p.dw.com/p/4UaD1
A view shows a destroyed building interior as clashes between the army and the paramilitary Rapid Support Forces (RSF) continue, in Omdurman
Picha: Mostafa Saied/REUTERS

Anga la Sudan lilifungwa kwa safari za kawaida za ndege baada ya kuzuka mgogoro wa kijeshi kati ya jeshi la nchi hiyo na vikosi vya wanamgambo wa RSF katikati ya Aprili.

Kwingineko, wanamgambo wa RSF waliwaamuru raia kuyahama makaazi yao kusini mwa mji mkuu Khartoum.

Soma zaidi: Mjumbe wa RSF asema ni wakati wa amani Sudan, Darfur

Wakaazi kadhaa walisema kuwa wanamgambo hao waliwaambia walikuwa na masaa 24 kuyahama makaazi yao.

Mamia ya wakaazi wanafurushwa kutoka kitongoji cha Jabra kilichopo kusini mwa Kahrtoum, ambako pamoja na eneo jirani la Sahafa ni makao ya jeshi la Sudan pamoja na kituo cha RSF kinachotumiwa na jenerali wa wanamgambo hao, Mohamed Hamdan Dagalo.