1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Mwanaharakati wa jamii ya LGBTQ nchini Uganda ashambuliwa

4 Januari 2024

Mwanaharakati maarufu wa haki za jamii inayojihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda Steven Kabuye amelazwa hospitalini akitibiwa baada ya kushambuliwa kwa visu.

https://p.dw.com/p/4aqSW
 Uganda yapinga sheria dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi wa jinsia moja
Wanaharakati wakiwa na mabango yenye ujumbe unaopinga muswada dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda mbele ya ubalozi wa taifa hilo mjini Pretoria, Afrika Kusini, Aprili 4, 2023. Wiki moja kabla, bunge la Uganda lilipitisha muswada wa kuipinga vitendo vinavyofanywa na jamii hiyo.Picha: Themba Hadebe/AP/picture alliance

Kulingana na jeshi la polisi la Uganda hali ya mwanaharakati huyo wa jamii ya LGBTQ ni mbaya sana.

Video kwenye mtandao wa X inamuonyesha Kabuye akiwa amelala chini na mwenye maumivu makali, jeraha kubwa la kisu kwenye mkono wa kulia na kisu kilichonasa tumboni.

Msemaji wa polisi Patrick Onyango amesema watu walimkuta Kabuye akiwa na hali mbaya baada ya kushambuliwa.

Kabuye amedai kwamba washambuliaji hao walinuia kumuua na si kumpora na kuongeza kuwa wamekuwa wakimfuatilia kwa siku kadhaa.

Wanaharakati wa jamii hiyo nchini Uganda wamekuwa wakielezea hofu yao tangu taifa hilo lilipopitisha sheria mpya dhidi ya jamii hiyo, wakisema itaongeza mashambulizi dhidi yao.