1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Myanmar kuwaruhusu raia 'watiifu' kubeba silaha

14 Februari 2023

Jeshi la Myanmar na vyombo vya habari vimeripoti kuwa utawala wa kijeshi unapanga kuwaruhusu watu waliotajwa kuwa waaminifu kwa taifa, wakiwemo wafanyakazi wa serikali na wanajeshi wastaafu kubeba silaha zenye leseni,

https://p.dw.com/p/4NSBb
Myanmar | Min Aung Hlaing
Picha: The Military True News Information Team via AP/picture alliance

Watu hao wanapaswa kutii maagizo kutoka kwa serikali za mitaa kushiriki hatua za utekelezaji wa sheria na usimamizi wa usalama. 

Tangazo hilo limechochea hofu ya kutokea ghasia zaidi katika nchihiyo iliyoharibiwa na kile ambacho baadhi ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamekiita vita vya wenyewe kwa wenyewe. 

Soma pia:Myanmar yatangaza hatua mpya kali dhidi ya 'habari za uongo'

Waraka wa kurasa 15 kuhusu sera mpya ya silaha unaohusishwa na wizara ya mambo ya ndani ulisambazwa awali kupitia akaunti za mtandao wa Facebook zinazounga mkono jeshi.

Jeshi liliipinduwa serikali iliyochaguliwakidemokrasia ya Aung San Suu Kyi miaka miwili iliyopita, na kusababisha maandamano ya amani yaliyoenea, ambayo yaligeuka kuwa upinzani wa silaha baada ya vikosi vya usalama kutumia nguvu kubwa kukandamiza upinzani wote.