1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Marekani lashambulia maeneo ya Wahouthi huko Yemen

Josephat Charo
20 Juni 2024

Vikosi vya Marekani vimeharibu maeneo mawili nchini Yemen yanayomilikiwa na waasi wa Houthi, jeshi la Marekani limesema, kufuatia mfululizo wa mashambulizi dhidi ya meli katika siku chache zilizopita.

https://p.dw.com/p/4hHMQ
Vikosi vya kamandi kuu ya jeshi la Marekani pamoja na majeshi ya Uingereza na wanaheshi kutoka Bahrain, Canada, Denmark,Uholanzi na New Zealand vikifanya mashambulizi dhidi ya maeneo 13 katika maeneo yanadhibitiwa  Australia, Uingereza, Canda, Denmark, Uholanzi na Zew Zealand
Picha: CENTCOM/Handout/Anadolu/picture alliance

Jeshi la Marekani limesema limekiharibu kituo kimoja cha udhibiti wa ardhini na kamandi moja katika eneo linalodhibitiwa na waasi wa Houthi nchini Yemen.

Katika taarifa yake kamandi kuu ya jeshi la Marekani imeongeza kwamba vikosi vyake pia vimeziharibu boti mbili za droni za Wahouthi katika bahari ya Shamu.

Waasi wa Houthi wanaoegemea Iran walianzisha mashambulizi ya droni na makombora katika njia muhimu ya baharini mnamo Novemba mwaka uliopita katika kile wanachosema ni kuonyesha mshikamano na wanamgambo wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Katika zaidi ya mashambulizi 70, Wahouthi wamefanikiwa kuzamisha meli mbili, kuiteka moja na kuwaua mabaharia kadhaa.