1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Jeshi la kikanda lajiondoa mji wa kimkati wa Shire-Tigray

13 Januari 2023

Jeshi la kikanda lililokuwa likiisaidia serikali ya Ethiopia katika vita vilivyodumu kwa miaka miwili dhidi ya waasi wa Tigray limejiondoa kutoka kwenye mji wa kimkakati wa Shire katika jimbo la Tigray.

https://p.dw.com/p/4M7GG
Äthiopien | Tigray Soldaten in Mekelle
Picha: Million Haile Selassie/DW

Jeshi la kikanda lililokuwa likiisaidia serikali ya Ethiopia katika vita vilivyodumu kwa miaka miwili dhidi ya waasi wa Tigray limejiondoa kutoka kwenye mji wa kimkakati wa Shire katika jimbo la Tigray.Taarifa ya jeshi imesema vikosi hivyo maalumu vya Amhara vimeondoka baada ya tangazo lililotolewa siku ya Jumatano na chama cha Ukombozi wa watu wa Tigray, TPLF kwamba wameanza kusalimisha silaha nzito. Hatua hiyo ni sehemu muhimu ya makubaliano ya amani ya Novemba mwaka jana kati ya serikali ya Ethiopia na TPLF ya kumaliza mzozo katika jimbo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia vilivyosababisha idadi kubwa ya vifo vya raia. Kwa muda mrefu wanamgambo wa Tigray wamekuwa wakishinikiza kuondoka kwa wanajeshi wa Eritrea waliokuwa na jukumu kubwa katika kulisaidia jeshi la Ethiopia kwenye vita hivyo.