1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Wapalestina 700,000 wametoroka eneo la Kaskazini la Gaza

21 Oktoba 2023

Jeshi la Israel limesema leo kuwa takriban Wapalestina 700,000 wametorokea eneo la Kusini mwa Gaza baada ya wito kutolewa kwa raia walioko katika eneo la Kaskazini la ukanda huo kuondoka kutoka eneo hilo

https://p.dw.com/p/4Xr6E
Shambulizi la Israel katika ukanda wa Gaza
Shambulizi la Israel katika ukanda wa GazaPicha: DW

Katika taarifa kupitia televisheni, msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari, amesema raia waliobaki katika mji wa Gaza City na maeneo ya Kaskazini ya ukanda huo, wanapaswa kuhamia maeneo ya Kusini ya hifadhi ya Wadi katika ukanda huo kwa usalama wao wenyewe.

Hagari aonya hatua zijazo za vita heunda zikawa tishio kwa jeshi la ardhini

Hagari ameonya kuwa Israel itaongeza mashambulizi yake katika ngome za kundi la Hamas na taasisi za serikali katika eneo la Kaskazini na mashambulizi hayo yanaweza kuwa tishio kwa vikosi vya ardhini katika hatua zijazo za vita hivyo.

Ni wiki mbili sasa tangu kundi la hamas lilipofanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya Israel na kusababisha vifo vya mamia ya watu. Tangu wakati huo, mashambulizi ya kisasi kutoka Israel kuelekea ukanda wa Gaza, yamesababisha hofu ya janga la kibinadamu na ongezeko la mvutano wa kikanda.