1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Wanajeshi zaidi wapeleka katika eneo la Ukingo wa Magharibi

21 Juni 2023

Jeshi la Israel limepeleka wanajeshi zaidi katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la nchi hiyo la Ukingo wa Magharibi na kujiandaa kubomowa makaazi ya wapalestina wawili waliokuwa na silaha waliowauwa Waisreli wanne

https://p.dw.com/p/4SskC
Westjordanland | Israelischer Militäreinsatz in Jenin
Picha: Nedal Eshtayah/AA/picture alliance

Wanamgambo hao wawili wakipalestina walifyetuwa risasi katika mgahawa mmoja ulioko kwenye kituo cha mafuta kwenye eneo hilo la Ukingo wa Magharibi na kuwauwa Waisraeli wanne.

Tukio hilo latokea siku moja baada ya Wapalestina saba kuuliwa

Tukio hilo limekuja siku moja baada ya wapalestina saba kuuliwa katika mapambano yaliyotokea siku nzima dhidi ya wanajeshi wa Israel katika mji wa Jenin ambao ni ngome ya wanamgambo wa Kipalestina. Leo jeshi la Israel limesema linaimarisha ulinzi katika Ukingo wa Magharibi huku pia likisema limewakamata washukiwa watatu katika kijiji cha Urif.