1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya kiutu Ukanda wa Gaza inaendelea kuwa mbaya

5 Desemba 2023

Jeshi la Israel limeendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza ambako hali ya kibinadamu hasa eneo la kusini ikikaribia kuwa 'mbaya zaidi'.

https://p.dw.com/p/4Zmig
Nahostkonflikt | Nablus
Picha: Issam Rimawi/AA/picture alliance

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema mateso ya watu wa Gaza 'hayavumiliki' na kutoa wito wa kuwepo suluhisho la kisiasa na kuhakikisha raia wanalindwa kwa mujibu wa sheria za vita na kuruhusu misaada kuingia Gazabila vikwazo. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema karibu watu milioni 1.9 ikiwa ni sawa na asilimia 80 ya wakazi wote huko Gaza wameyakimbia makazi yao tangu kuanza kwa vita hivyo Oktoba 7.