1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel laushambulia vikali Ukanda wa Gaza

8 Julai 2024

Majeshi ya Israel yameshambulia kwa vifaru mapema maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, katika kile ambacho wakazi wamesema ilikuwa moja ya mashambulizi makali zaidi tangu Oktoba 7.

https://p.dw.com/p/4i0b4
Vita vya Mashariki ya Kati
Israel yaendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa GazaPicha: Omar Ashtawy/APA/IMAGO

Huduma za Dharura kwenye eneo hilo zimesema wanaamini kuwa watu kadhaa waliuawa katika maeneo ya mashariki mwa Gaza lakini hawakuweza kuwafikia watu hao kutokana na mashambulizi yanayoendelea huko Tel Al-Hawa, Sabra, Daraj, Rimal, na vitongoji vya Tuffah.

Netanyahu kupeleka wawakilishi majadiliano ya kusitisha vita Gaza

Jeshi la Israel limesema liliendesha operesheni dhidi ya miundombinu ya wapiganaji huko Gaza, na kwamba limewatokomeza wapiganaji 30 ambao linadai walikuwa tishio kwa wanajeshi wake.