1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la anga la Nigeria lakiri kuhusika na shambulizi

28 Januari 2024

Jeshi la anga la Nigeria limesema linajutia shambulio lake lililowaua makumi ya raia na kuwajeruhi wengine mwaka mmoja uliopita, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa jeshi hilo kukubali kuhusika katika tukio hilo.

https://p.dw.com/p/4bleT
Wanajeshi wa Nigeria
Wanajeshi wa Jeshi la NigeriaPicha: Reuters

Jeshi hilo limesema kuwa Kiongozi wake wa ngazi ya juu Hasan Abubakar alizitembelea jamii zilizoathiriwa na shambulio hilo baada ya kuhakikisha ripoti za mkasa huo.

 Aboubakar alisema kuwa mashambulizi hayo hayakufanywa kwa makusudi bali yaliwalenga magaidi na wezi wa mifugo kutokana na ongezeko la ukosefu wa usalama katika eneo hilo kwa wakati huo.

Soma pia: Watu 30 wauawa Nigeria

Itakumbukwa kuwa, mwezi Januari mwaka 2023, makumi ya wafugaji wa kabila la Fulani waliuwawa katikati mwa jimbo la Nasarawa baada ya kushambuliwa kwa mabomu yaliyoporomoshwa kwa njia ya anga.

Soma pia: Watu 113 wauawa katika mashambulizi katikati mwa Nigeria

Jeshi la anga limesema kukutana na wawakilishi wa wahaathiriwa wa shambulio hilo "kutasaidia katika kujibu baadhi ya maswali muhimu, kuboresha uwajibikaji, uwazi" na kuzuia matukio kama hayo katika siku zijazo. Hata hivyo suala la fidia halikutajwa.