1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Israel yakubali azimio la Umoja wa Mataifa juu ya kusimamisha mapigano

13 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDLt

Baraza la mawaziri la Israel limeidhinisha azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kusimamisha mapigano nchini Lebanon.

Msemaji wa serikali ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mawaziri 24 walipiga kura ya ndiyo kulipitisha azimio hilo namba 1701 .Waziri mmoja hakupiga kura.

Waziri mkuu Ehud Olmert amesema kuwa azimio hilo ni jambo zuri kwa Israel.

Azimio hilo litaanza kutekelezwa kesho.

Hatahivyo majeshi ya Israel na wapiganaji wa Hezbollah waliaendelea kupambana kusini mwa Lebanon.