1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Wahamiaji watarejeshwa walikopitia

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXi

Israel hii leo imearifu kuwa haitowaruhusu wakimbizi kutoka eneo la mgogoro la Darfur kuingia Israel,lakini kiasi ya wakimbizi 500 ambao tayari wapo nchini humo wataruhisiwa kubakia kwa sababu za kiutu.Azma ya siasa hiyo ni kuzuia uhamiaji haramu kutoka Afrika kwa kupitia Misri.

Msemaji wa serikali ya Israel,David Baker ameeleza kuwa siasa ya Israel ni kwamba ye yote atakaeingia kutoka Misri kwa njia isiyo halali, atarejeshwa Misri.Kwa mujibu wa makundi yanayopigania haki za binadamu,katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita,zaidi ya wahamiaji 2,000 kutoka Afrika wamejipenyeza Israel kwa njia zisizo halali kwa kupitia Misri,wakitafuta maisha bora.