1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel huenda iyaondoe makazi ya wayahudi mapema

21 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEs7

Israel imesema mpango wake wa kuyaondoa makazi ya walowezi wa kiyahudi kutoka mkanda wa Gaza huenda ufanyike mapema. Naibu wa waziri mkuu, Ehud Olmert, amesema katika redio ya Israel kwamba mpango huo ambao ulitarajiwa kuanza katikati ya mwezi Agosti huenda ufanyike mapema kuzuia kutokea kwa maandamano mengine.

Tangazo hili amelitoa baada ya waandamanaji wanaoupinga mpango huo kumaliza maandamano yao. Olmert amesema jambo hilo litajadiliwa katika mazungumzo kati ya waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice.