1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jenerali jeshi la Ujerumani ataka wanawake watumikie jeshi

4 Julai 2024

Inspekta mkuu wa majeshi ya Ujerumani amependekeza kwamba wanawake wajumuishwe kwenye sheria ya kutumikia jeshi kwa lazima ikiwa sheria hiyo itarejeshwa ili kuweka usawa.

https://p.dw.com/p/4hqJK
Carsten Breuer, inspekta mkuu wa jeshi la Ujerumani.
Carsten Breuer, inspekta mkuu wa jeshi la Ujerumani.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Afisa huyo wa ngazi za juu kabisa jeshini, Carsten Breuer, ameliambia shirika la habari la RND kwenye mahojiano yaliyochapishwa leo kwamba, kwa ilivyo sasa, sheria hiyo inawahusu wanaume pekee.

Ujerumani iliindosha rasmi kuwaandikisha watu jeshini kwa lazima mwaka 2011, ingawa sheria hiyo inaendelea kutumika kwenye mazingira ya vita.

Uvamizi wa kijeshi wa Urusi dhidi ya Ukraine umelifanya jeshi la Ujerumani kufikiria uwezekano wa kurejesha amri ya watu wote kutumikia jeshini kwa lazima. Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius aliwasilisha mipango ya utumishi jeshini mwezi uliopita kusaidia kujaza nafasi tupu.