1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je,kauli ya Spika Ndugai inatokana na shinikizo la CCM?

Hawa Bihoga3 Januari 2022

Baada ya Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai kumuomba radhi Rais Samia Suluhu na Watanzania kutokana na kile alichokitaja kauli yake kugeuzwa na watu wasiokuwa na nia njema, baadhi ya wachambuzi wanasema hatua hiyo inatokana na shinikizo kubwa la ndani ya chama chake pamoja na kujitafakari kama kiongozi. Masele Hamdun,ni mchambuzi wa masuala ya siasa kutoka Tanzania.

https://p.dw.com/p/455ea

Baada ya Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai kumuomba radhi Rais Samia Suluhu na Watanzania  kutokana na kile alichokitaja kauli yake kugeuzwa na watu wasiokuwa na nia njema, baadhi ya wachambuzi wanasema hatua hiyo inatokana na shinikizo kubwa la ndani ya chama chake pamoja na kujitafakari kama kiongozi. Baada ya Spika Ndugai kutoa kauli ilionesha kupinga juhudi za Rais Samia kukopa fedha kwa ajili ya kufanya miradi ya kimaendeleo, baadhi ya viongozi wa chama tawala CCM katika mikoa mbalimbali walijitokeza na kupinga wazi kauli hiyo ilioonesha kukosoa uamuzi huo wa mamlaka. Hawa Bihoga amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisaisa Masele Hamdun kutoka Mwanza Tanzania na kwanza anaanza kumuelezea tathmini yake juu ya hatua hiyo ya Spika Ndugai.