1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, maandamano ya Kenya yamepoteza dira?

3 Julai 2024

Wanaharakati wanaoongoza maandamano wamesema wanafikiria njia mbadala ya kupaza sauti zao baada ya maandamano yao kuingiliwa na watu waliowaita majambazi. Wanaharakati hao wamedai wahalifu wameletwa na wanasiasa kuharibu muelekeo wa maandamano ya vijana maarufu kama Gen Z. Amina Abubakar amezungumza na Alutalala Mukhwana, mchambuzi wa siasa nchini Kenya juu ya muelekeo wa sasa wa maandamano hayo.

https://p.dw.com/p/4hp4N