1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaJapan

Japan yatangaza tahadhari ya tsunami

1 Januari 2024

Nyumba zipatazo 33,500 hazina umeme katika eneo ambalo limepigwa na mfululizo wa matetemeko makubwa ya chini ya bahari nchini Japan ambayo athari zake zimeshuhudiwa hadi kwenye miji ya mashariki ya mbali ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4alwK
Nyufa zinaoekana ardhini mjini Wajima Japan kufuatia tetemeko la ardhi.
Nyufa zinaoekana ardhini mjini Wajima Japan kufuatia tetemeko la ardhi.Picha: Kyodo News/AP/picture alliance

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Japan imesema tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.6 kwa kipimo cha Richter limeathiri zaidi miji ya Toyama, Ishikawa na Niigata, yote kwenye kisiwa chake kikubwa cha Honshu kilicho kwenye mwambao wa magharibi wa Bahari ya Japan.

Shirika la habari la Urusi, TASS, limewanukuu mameya wa miji ya Vladivostok na Nakhodka wakitangaza tahadhari ya tsunami katika maeneo hayo yaliyo kwenye kisiwa cha Sakhalin.

Soma pia: Istanbul yapigwa na tetemeko la ardhi

Onyo la mawimbi yenye ukubwa wa mita tatu lilitolewa pia kwenye baadhi ya maeneo ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.

Serikali mjini Seoul iliwataka wakaazi wa miji ya mwambao wa mashariki kuchukuwa tahadhari ya kupanda kwa viwango vya bahari.