1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Maji ya bahari karibu na kinu cha Fukushima ni salama

27 Agosti 2023

Wizara ya mazingira ya Japan imesema vipimo vya maji ya bahari karibu na kinu cha nyuklia cha Fukushima havionyeshi kuwepo na mionzi ya nyuklia.

https://p.dw.com/p/4VcS1
Wanaharakati wa Korea Kusini wakiwa na mabango yanayolenga kuizuia Japan kuchafua maji ya bahari kwa kutiririsha maji ya Fukushima
Japan imekabiliwa na ukosoaji mkali baada ya hatua yake ya kuanza kutiririsha maji ya kwenye kinu cha nyuklia cha Fukushima kuelekea bahariniPicha: Minwoo Park/REUTERS

Wizara ya mazingira ya Japan imesema haya siku kadhaa baada ya mamlaka kuanza kutiririsha maji yaliyosafishwa kutoka kinu hicho kwenda baharini na kuondolewa viambata vya mionzi.

Wizara hiyo imesema vipimo vimeonyesha kuwa kiwango cha chini cha mionzi ambacho hakina athari yoyote mbaya kwa afya ya binaadamu na mazingira.

Japan ilianza kutirirsha maji kutoka kwenye kinu hicho cha Fukushima kilichoharibiwa na janga la Tsunami la mnamo mwaka 2011, hatua iliyoibua ukosoaji nchini huimo na mataifa jirani na hasa China.

Kulingana na wizara hiyo, watakuwa wakichapisha matokeo ya vipimo kama hivi kila wiki katika kipindi cha angalau miezi mitatu.