1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan kujiandaa na kitisho cha Korea

22 Aprili 2023

Waziri wa Ulinzi wa Japan Yasukazu Hamada ametoa amri ya kwa kikosi cha kujihami cha nchi hiyo kujiandaa kuiangusha satelaiti ya kijasusi ya Korea Kaskazini

https://p.dw.com/p/4QR8b
USA und Japan Verteidigungsminister Treffen in Washington DC
Picha: Joshua Roberts/REUTERS

Waziri wa Ulinzi wa Japan Yasukazu Hamada ametoa amri ya kwa kikosi cha kujihami cha nchi hiyo kujiandaa kuiangusha satelaiti ya kijasusi ya Korea Kaskazini iwapo itatokea kuingia katika anga ya Japan.Kwa mjibu wa Shirika la Habari la Japan-Kyodo likinuu chanzo kutoka serikali ya Japan amri hiyo ya Hamada imetolewa leo.Awali Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alisema maandalizi ya uzinduzi uliopangwa wa satelaiti ya kwanza ya kijasusi nchini humo unapaswa kufanyika kwa ajili ya kuendelea kukabiliana na vitisho kutoka kwa Marekani na Korea Kusini.