1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA : Waustralia wanne wahukumiwa kifo

6 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEo

Mahkama Kuu ya Indonesia imewahukumu kifo vijana wanne wa Australia kwa kuvusha kwa magendo mihadarati na kubatilisha hukumu za awali za vifungo gerezani hatua ambayo yumkini ikavuruga uhusiano katika ya nchi mbili hizo jirani.

Zarof Ricar mkurugenzi wa sheria ya jinai katika Mahkama Kuu amesema vijana watatu wamehukumiwa kifo baada ya waendesha mashataka wa serikali kukata rufaa dhidi ya kupunguzwa kwa hukumu zao za vifungo.

Muastralia wa nne pia amehukumiwa kifo baada ya kukata rufaa dhidi ya hukumu ya awali ambayo pia ilikuwa ni ya kifo.

Kwa mujibu wa maafisa wa mahkama watu sita wa kile kinachoitwa Kundi la Watu Tisa la Bali walikamatwa kwenye eneo la mapumziko ya kitalii la kisiwa cha Bali mwaka jana wakati wakijaribu kuvusha kwa magendo zaidi ya kilo 8.2 za madawa ya kulevya kwenda Australia hivi sasa wanakibiliwa na hukumu ya kifo.